Add parallel Print Page Options

17 Onesheni heshima kwa watu wote: Wapendeni ndugu zenu na dada zenu waliomo nyumbani mwake Mungu. Mcheni Mungu na mumheshimu mfalme.

Mfano wa Mateso ya Kristo

18 Watumwa mlio nyumbani, watumikieni mabwana wenu kwa heshima yote,[a] siyo tu wale walio wapole na wenye busara, bali hata wale walio wakali. 19 Baadhi yenu mtapata mateso wakati ambapo hamjafanya kosa lolote. Ikiwa utaweza kuvumilia maumivu na kuweka fikra zako kwa Mungu, hilo linampendeza sana Mungu.

Read full chapter

Footnotes

  1. 2:18 kwa heshima yote Au “kwa heshima na taadhima kwa Mungu”.