Jiwe Hai Na Taifa Takatifu

Basi, njooni kwake yeye aliye Jiwe lililo hai, ambalo lili kataliwa na watu bali kwa Mungu ni teule na la thamani kubwa. Ninyi pia, kama mawe hai mjengwe kuwa nyumba ya kiroho, mpate kuwa makuhani watakatifu, mkitoa sadaka za kiroho zinazokubaliwa na Mungu kwa njia ya Yesu Kristo. Kwa maana imeandikwa katika Maandiko: “Tazama, ninaweka jiwe kuu la msingi huko Sayuni; jiwe la pembeni teule na la thamani kubwa, na kila amwaminiye hataaibika.”

Read full chapter