Font Size
1 Petro 2:5-7
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
1 Petro 2:5-7
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
5 Ninyi pia, kama mawe yaliyo hai mnajengwa ili kuwa hekalu la kiroho. Mmekuwa makuhani watakatifu mkimtumikia Mungu kwa kutoa sadaka za kiroho zinazokubalika kwake kwa njia ya Yesu Kristo. 6 Hivyo, Maandiko yanasema,
“Tazameni, naweka katika Sayuni Jiwe la msingi katika jengo,
lililoteuliwa na kuheshimika,
na yeyote anayeamini hataaibishwa.”(A)
7 Inamaanisha heshima kwenu mnaoamini, bali kwa wasioamini,
“jiwe walilolikataa wajenzi
limekuwa jiwe la muhimu kuliko yote.”(B)
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)
© 2017 Bible League International