Kwenu ninyi mnaoamini, yeye ni wa thamani kubwa. Lakini kwao wasioamini, “Lile jiwe walilokataa waashi limekuwa jiwe kuu la msingi,” na, “Jiwe ambalo litawafanya watu wajik wae; mwamba ambao utawafanya waanguke.” Wanajikwaa kwa sababu hawatii lile neno, kama walivyopangiwa tangu mwanzo.

Lakini ninyi ni uzao mteule, ukuhani mtukufu, taifa taka tifu, watu pekee wa Mungu mlioteuliwa kutangaza matendo makuu ya aliyewaita kutoka gizani na kuwaingiza katika nuru yake ya ajabu.

Read full chapter