Lakini ninyi ni uzao mteule, ukuhani mtukufu, taifa taka tifu, watu pekee wa Mungu mlioteuliwa kutangaza matendo makuu ya aliyewaita kutoka gizani na kuwaingiza katika nuru yake ya ajabu. 10 Hapo mwanzo ninyi mlikuwa si taifa, lakini sasa ninyi ni watu wa Mungu. Hapo mwanzo mlikuwa hamjapata rehema, lakini sasa mme pata rehema.

11 Rafiki wapendwa, ninawasihi, mkiwa kama wageni na wapi taji njia hapa duniani, epukeni tamaa mbaya za mwili ambazo hupi gana vita na roho zenu.

Read full chapter