Add parallel Print Page Options

Lakini ninyi ni watu mlioteuliwa, ni Ukuhani unaomtumikia Mfalme. Ninyi ni taifa takatifu nanyi ni watu wa Mungu. Yeye aliwaita Ili muweze kutangaza matendo yake yenye nguvu. Naye aliwaita mtoke gizani na mwingie katika nuru yake ya ajabu.

10 Kuna wakati hamkuwa watu,
    lakini sasa mmekuwa watu wa Mungu.
Kuna wakati hamkuoneshwa rehema,
    lakini sasa mmeoneshwa rehema za Mungu.

Mwishie Mungu

11 Rafiki zangu, ninawasihi kama wapitaji na wageni katika ulimwengu huu kuwa mbali na tamaa za kimwili, ambazo hupingana na roho zenu.

Read full chapter