10 awe mwenye sifa ya matendo mema, aliyewalea watoto wake vizuri, aliyekuwa mkarimu, aliyewaosha miguu watu wa Mungu, ali yewasaidia watu wenye taabu na aliyejitolea kufanya mema kwa kila njia. 11 Lakini wajane vijana usiwaweke kwenye orodha hiyo, maana tamaa zao za kimaumbile zikizidi kule kujitoa kwao kwa Kristo, watataka kuolewa tena. 12 Na kwa njia hiyo watajiletea hukumu kwa kuivunja ahadi yao ya mwanzo.

Read full chapter