Add parallel Print Page Options

Maagizo maalumu kwa Watumwa

Wote ambao ni watumwa waoneshe heshima kubwa kwa mabwana zao. Ndipo jina la Mungu na mafundisho yetu hayatakosolewa. Baadhi ya watumwa wanao mabwana ambao ni waamini, hivyo hao ni ndugu. Je, inamaanisha wasiwaheshimu mabwana zao? Hapana, watawatumikia hata kwa uzuri zaidi, kwa sababu wanawasaidia waaminio, watu wawapende.

Haya ni mambo ambayo lazima uyafundishe na kumwambia kila mtu kufanya.

Mafundisho ya Uongo na Utajiri wa Kweli

Watu wengine wanafundisha uongo na hawakubaliani na mafundisho ya kweli ambayo yanatoka kwa Bwana wetu Yesu Kristo. Hawakubali mafundisho ambayo yanatuongoza kumheshimu na kumpendeza Mungu.

Read full chapter