Add parallel Print Page Options

Ninaweza kutoa kila kitu nilichonacho ili niwasaidie wengine na ninaweza hata kuutoa mwili wangu ili niweze kujisifu.[a] Lakini siwezi kupata chochote kwa kufanya haya yote ikiwa sina upendo.

Upendo huvumilia na ni mwema. Upendo hauna wivu, haujisifu na haujivuni. Upendo hauna kiburi, hauna ubinafsi na haukasirishwi kirahisi. Upendo hautunzi orodha ya mambo waliyoukosea.

Read full chapter

Footnotes

  1. 13:3 kuutoa mwili wangu ili niweze kujisifu Kwa maana ya kawaida, “ili nichomwe moto”, ambayo inapatikana katika nakala za kale na bora zaidi za Kiyunani. Baadhi ya nakala za kale za Kiyunani zimetumia hapa maneno “hata nikichomwa moto”, kwa maana hii ya “Kujisifu”, tazama 2 Kor 12:9-10.