Add parallel Print Page Options

kwa sababu kila ambae ni mwana wa Mungu ana uwezo wa kushinda dhidi ya ulimwengu. Ni imani yetu iliyoshinda vita dhidi ya ulimwengu. Hivyo ni nani anayeushinda ulimwengu? Ni wale tu wanaoamini kuwa Yesu ni mwana wa Mungu.

Mungu alituambia kwa Habari ya Mwanae

Yesu Kristo ndiye aliyekuja. Alikuja kwa maji na damu.[a] Hakuja kwa maji peke yake. Lahasha, Yesu alikuja kwa vyote maji na damu. Na Roho atuambia kuwa hili ni kweli. Roho ndiye Kweli.

Read full chapter

Footnotes

  1. 5:6 maji na damu Inaweza kumaanisha Maji ya ubatizo wa Yesu Kristo, na damu aliyo imwaga pale msalabani.