Kwa Timotheo, mwanangu mpendwa. Ninakutakia neema, rehema na amani kutoka kwa Mungu Baba na kwa Kristo Yesu Bwana wetu.

Paulo Amtia Moyo Timotheo

Ninamshukuru Mungu ninayemtumikia kwa dhamiri safi, kama walivyomtumikia baba zangu, ninapokukumbuka usiku na mchana katika sala zangu. Nikiyakumbuka machozi yako, ninatamani sana kukuona ili nijazwe furaha.

Read full chapter