Na sasa, mama mpendwa, sikuandikii amri mpya, bali ile ile ambayo tumekuwa nayo kutoka mwanzo: kwamba tupendane. Na upendo ni huu: kwamba tuishi kwa kuzifuata amri za Mungu. Na kama mlivyosikia tangu mwanzo, amri yake ni kwamba muishi maisha ya upendo.

Kwa maana wadanganyifu wengi wametokea duniani, watu wasiokiri ya kwamba Kristo alikuja kama mwanadamu. Mtu kama huyo ni mdanganyifu na mpinga-Kristo.

Read full chapter