Na upendo ni huu: kwamba tuishi kwa kuzifuata amri za Mungu. Na kama mlivyosikia tangu mwanzo, amri yake ni kwamba muishi maisha ya upendo.

Kwa maana wadanganyifu wengi wametokea duniani, watu wasiokiri ya kwamba Kristo alikuja kama mwanadamu. Mtu kama huyo ni mdanganyifu na mpinga-Kristo. Jihadharini msije mkapoteza yale mliyoyafanyia kazi, bali mpewe thawabu kamili.

Read full chapter