Add parallel Print Page Options

Walimu wengi wa uongo wamo duniani sasa. Wana kataa kusema Yesu ni Masihi aliyekuja duniani na kufanyika mwanadamu. Kila anayekataa kuikubali kweli hii ni mwalimu wa uongo na adui wa Kristo. Muwe waangalifu! Msiipoteze thawabu tuliyokwisha[a] kuitendea kazi. Mhakikishe mnaipokea thawabu kamili.

Kila mmoja aendelee kuyashika mafundisho aliyefundishwa juu Kristo tu. Yeyote atakayeyabadili mafundisho hayo hana Mungu. Kila anayeendelea kuyafuata mafundisho ya Kristo[b] anao wote Baba na Mwanaye.

Read full chapter

Footnotes

  1. 1:8 tuliyokwisha Nakala zingine za Kiyunani zina “mliyoyatenda”.
  2. 1:9 mafundisho ya Kristo Hii ilihusu mafundisho juu ya Kristo kama alikuwa mwanadamu na pia Mungu na pia mafundisho ambayo Kristo mwenyewe aliyafundisha.