Add parallel Print Page Options

Salamu toka kwa mzee.[a]

Kwa rafiki mpendwa gayo, mtu ni mpendae kwa dhati.

Rafiki yangu mpendwa, najua kwamba unaendelea vizuri kiroho, kwa hiyo ninaomba kuwa mengine yote yaendelee vizuri pia nawe uwe na afya njema. Baadhi ya waamini walikuja na kunieleza juu ya kweli[b] iliyo katika maisha yako. Waliniambia kuwa unaendelea kuifuata njia ya kweli. Hili lilinifanya nijisikie furaha sana.

Read full chapter

Footnotes

  1. 1:1 mzee Huyu huenda alikuwa ni Mtume Yohana. “Mzee” ina maana ya mtu aliye mtu mzima au kiongozi maalumu katika kanisa (kama vile katika Tit 1:5).
  2. 1:3 kweli Kweli au “habari njema” za Yesu Kristo zinazo waunganisha waamini wote pamoja. Pia katika mstari wa 8,12.