12 Baada ya haya, Yesu pamoja na mama yake, ndugu zake na wanafunzi wake, walikwenda Kapernaumu ambapo alikaa kwa siku chache.

Yesu Alitakasa Hekalu

13 Ilipokaribia sikukuu ya Wayahudi iitwayo Pasaka, Yesu alikwenda Yerusalemu. 14 Alipoingia Hekaluni aliwakuta watu wakiuza ng’ombe, kondoo na njiwa, na wengine wamekaa kwenye meza zao wakifanya biashara ya kubadilishana fedha. 15 Akatengeneza mjeledi wa kamba akawafukuza wote kutoka Hekaluni pamoja na kon doo na ng’ombe; akazipindua meza za wale waliokuwa wakibadilish ana fedha na kuzimwaga fedha zao. 16 Akawaambia wale waliokuwa wakiuza njiwa, “Watoeni hapa! Mnathubutuje kuifanya nyumba ya Baba yangu kuwa soko?” 17 Wanafunzi wake wakakumbuka kuwa Maan diko yalisema: “Upendo wangu kwa nyumba yako utaniangamiza.”

18 Viongozi wa Wayahudi wakamwuliza, “Unaweza kutuonyesha ishara gani kuthibitisha una mamlaka ya kufanya mambo haya?”

19 Yesu akawajibu, “Livunjeni hili Hekalu, nami nitalijenga tena kwa siku tatu!”

20 Wale Wayahudi wakamjibu, “Hekalu hili lilijengwa kwa muda wa miaka arobaini na sita. Wewe unasema unaweza kulijenga kwa siku tatu?”

21 Lakini yeye aliposema ‘Hekalu’ alikuwa anazungumzia mwili wake. 22 Kwa hiyo alipofufuliwa kutoka kwa wafu, wanafunzi wake walikumbuka maneno haya; wakayaamini Maandiko na yale maneno ali yosema Yesu.

Read full chapter