11 ‘Hata mavumbi ya mji wenu yaliyoko miguuni mwetu tunayakung’uta juu yenu; lakini fahamuni ya kwamba Ufalme wa Mungu umekuja karibu yenu!’ 12 “Nawahakikishia kwamba siku ile Mungu atakapouhukumu ulimwengu adhabu ya Sodoma itakuwa nafuu kuliko ya mji huo! 13 Ole wenu watu wa Korazini na wa Bethsaida! Kwa maana kama miujiza iliyofanyika kwenu ingalifany ika Tiro na Sidoni watu wa huko wangalitubu zamani, wakivaa magu nia na kujimwagia majivu kama dalili ya majuto.

Read full chapter