Add parallel Print Page Options

32 Kisha Mlawi[a] alipokaribia na kumwona yule mtu, alipita upande mwingine. Hakusimama ili amsaidie, Alikwenda zake.

33 Ndipo Msamaria[b] mmoja aliyekuwa anasafiri kupitia njia ile ile, alipofika mahali ambapo mtu aliyejeruhiwa alikuwa amelala, alipomwona alimhurumia. 34 Alimkaribia ili amsaidie, akamsafisha majeraha kwa mafuta ya zeituni na divai,[c] kisha akayafunga majeraha yake. Msamaria alikuwa na punda. Akampandisha juu ya punda wake na kumpeleka mpaka kwenye nyumba ya wageni. Akamhudumia huko.

Read full chapter

Footnotes

  1. 10:32 Mlawi Yaani mtumishi wa Hekalu.
  2. 10:33 Msamaria Wayahudi waliwachukulia Wasamaria kama maadui. Tazama Msamaria katika Orodha ya Maneno.
  3. 10:34 mafuta ya zeituni na divai Vilitumika kama dawa kwa ajili ya kulainisha na kusafisha majeraha.