Add parallel Print Page Options

33 Ndipo Msamaria[a] mmoja aliyekuwa anasafiri kupitia njia ile ile, alipofika mahali ambapo mtu aliyejeruhiwa alikuwa amelala, alipomwona alimhurumia. 34 Alimkaribia ili amsaidie, akamsafisha majeraha kwa mafuta ya zeituni na divai,[b] kisha akayafunga majeraha yake. Msamaria alikuwa na punda. Akampandisha juu ya punda wake na kumpeleka mpaka kwenye nyumba ya wageni. Akamhudumia huko. 35 Siku iliyofuata, Msamaria alitoa sarafu mbili za fedha na kumpa mtunza nyumba ya wageni, akamwambia, ‘Mtunze mtu huyu aliyejeruhiwa. Ukitumia pesa nyingi zaidi kwa kumhudumia, nitakulipa nitakapokuja tena.’”

Read full chapter

Footnotes

  1. 10:33 Msamaria Wayahudi waliwachukulia Wasamaria kama maadui. Tazama Msamaria katika Orodha ya Maneno.
  2. 10:34 mafuta ya zeituni na divai Vilitumika kama dawa kwa ajili ya kulainisha na kusafisha majeraha.