Taa Ya Mwili

33 “Hakuna mtu awashaye taa akaificha au kuifunika, ila huiweka mahali pa juu ili watu wote wanaoingia waone nuru yake. 34 Jicho lako ni nuru ya mwili wako. Macho yakiwa mazima huan gaza mwili wako wote; lakini yakiwa mabovu, mwili wako pia uta kuwa katika giza. 35 Kwa hiyo hakikisha kwamba una nuru ndani yako, wala si giza.

Read full chapter