35 Kwa hiyo hakikisha kwamba una nuru ndani yako, wala si giza. 36 Ikiwa mwili wako wote una nuru, bila sehemu yo yote kuwa gizani, basi utang’aa kabisa kama inavyokuwa wakati taa inapokuangazia.”

Yesu Awaonya Mafarisayo Na Wanasheria

37 Yesu alipomaliza kuzungumza, Farisayo mmoja alimkaribisha nyumbani kwake kwa chakula. Yesu akaingia na kuketi chakulani moja kwa moja.

Read full chapter