39 Ndipo Bwana akamwambia, “Ninyi Mafarisayo mnasafisha kikombe na sahani kwa nje huku ndani mmejaa udhalimu na uovu. 40 Wajinga Ninyi! Hamjui kuwa yeye aliyetengeneza sehemu ya nje ndiye aliyetengeneza na ya ndani pia? 41 Watendeeni ukarimu maskini kwa kuwapa vilivyomo ndani ya vikombe na sahani zenu na kila kitu kitakuwa safi kwenu.

Read full chapter