Font Size
Luka 11:42-44
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Luka 11:42-44
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
42 Lakini, ole wenu ninyi Mafarisayo! Mnampa Mungu sehemu ya kumi ya vyakula mnavyopata, hata mnanaa, na hata kila mmea mdogo katika bustani[a] zenu. Lakini mnapuuzia kuwatendea haki wengine na kumpenda Mungu. Haya ni mambo mnayotakiwa kufanya. Na endeleeni kufanya mambo hayo mengine.
43 Ole wenu ninyi Mafarisayo, kwa sababu mnapenda kupata viti vya heshima katika masinagogi. Na mnapenda kusalimiwa na watu kwa kuheshimiwa sehemu za masoko. 44 Ole wenu, kwa kuwa mnafanana na makaburi ya zamani yasiyoonekana, ambayo watu hupita juu yake na kuyakanyaga bila kuyatambua.”
Read full chapterFootnotes
- 11:42 Mnampa … bustani Kwa maana ya kawaida, “Mnatoa zaka za mnanaa, mchicha na kila aina ya mboga mboga.” Sheria ya Musa iliwataka Waisraeli kushirikiana chakula kwa kutenga sehemu ya kumi ya mazao na mifugo yao kwa ajili ya Mungu (tazama Law 27:30-32; Kum 26:12). Hii haikujumuisha mazao madogo ya bustani kama yaliyotajwa hapa. Hivyo Mafarisayo hawa walikuwa wanatoa zaidi ya inavyotakiwa ili kuhakikisha kuwa hawavunji sheria.
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)
© 2017 Bible League International