15 Ndipo akawaambia, “Jihadharini na jilindeni na aina zote za choyo. Kwa maana uhai wa mtu hautokani na wingi wa mali aliyo nayo.”

16 Kisha akawaambia mfano, “Shamba la tajiri mmoja lilizaa sana. 17 Akawaza moyoni mwake, ‘Nifanye nini? Maana sina mahali pa kuweka mavuno yangu.’

Read full chapter