25 Na ni nani kati yenu ambaye kwa kujihangaisha anaweza kujiongezea urefu wa maisha yake hata kwa saa moja? 26 Kama hamwezi kufanya jambo dogo kama hilo; kwa nini basi mhangaikie hayo mengine? 27 Yata zameni maua yanavyostawi: hayafanyi kazi, wala kujitengenezea nguo; lakini ninawaambia, hata Sulemani katika ufahari wake wote, hakuwahi kuvishwa vizuri kama ua mojawapo!

Read full chapter