Add parallel Print Page Options

26 Na ikiwa hamwezi kufanya mambo madogo, kwa nini mnajihangaisha kwa mambo makubwa?

27 Yatafakarini maua yanavyoota. Hayafanyi kazi wala kujitengenezea mavazi. Lakini ninawaambia hata Sulemani, mfalme mkuu na tajiri, hakuvikwa vizuri kama maua haya. 28 Ikiwa Mungu huyavika vizuri namna hii majani ya porini, mnadhani atawafanyia nini ninyi? Hilo ni jani tu, siku moja li hai na siku inayofuata linachomwa moto. Lakini Mungu huyajali kiasi cha kuyapendezesha. Hakika atafanya zaidi kwa ajili yenu. Imani yenu ni ndogo!

Read full chapter