Lakini nitawaambia nani wa kumwogopa: mwogopeni yule ambaye baada ya kumwua mtu ana mamlaka ya kumtupa motoni. Naam: huyo, mwogopeni! Mnajua kwamba mbayuwayu watano huuzwa kwa bei ndogo sana. Lakini Mungu anamjali kila mmoja wao. Mungu anafahamu hata idadi ya nywele zilizoko katika vichwa vyenu. Kwa hiyo msiogope: ninyi mna thamani zaidi kuliko mbayuwayu wengi.

Read full chapter