10 Siku moja ya sabato, Yesu alikuwa akifundisha katika sinagogi mojawapo. 11 Na hapo alikuwapo mwanamke mmoja alikuwa ameugua kwa muda wa miaka kumi na minane kutokana na pepo ali yekuwa amemwingia. Hali hiyo ilimfanya mwanamke huyo apindike hata asiweze kusimama wima. 12 Yesu alipomwona, akamwita akam wambia, “Mama, uwe huru, umepona ugonjwa wako.”

Read full chapter