13 Yesu akamwekea mikono, na mara akasimama wima, akamtukuza Mungu. 14 Mkuu wa sinagogi akakasirika kwa kuwa Yesu alikuwa ameponya mtu siku ya sabato. Kwa hiyo akawaambia watu, “Kuna siku sita ambazo watu wanapaswa kufanya kazi, katika siku hizo, njooni mpo nywe; msije kuponywa siku ya sabato!”

15 Lakini Bwana akamjibu, “Ninyi ni wanafiki! Kila mmoja wenu humfungulia ng’ombe wake au punda wake kutoka zizini akampeleka kumnywesha maji siku ya sabato.

Read full chapter