24 Akajibu, “Jitahidini kuingia kwa kupitia mlango mwembamba; kwa maana, nawaambia, wengi watataka kuingia na hawataweza. 25 Wakati mwenye nyumba ataka poamka na kufunga mlango, mtasimama nje mkigonga mlango na kusema, ‘Bwana utufungulie!’ Atawajibu, ‘Sijui mtokako!’ 26 Nanyi mtamjibu, ‘Tulikula na kunywa pamoja nawe, ulifundisha katika mitaa yetu!’

Read full chapter