13 Hakuna mtumishi awezaye kuwatumikia mabwana wawili. Ama atamchukia mmoja na kumpenda mwingine; au atamheshimu mmoja na kumdharau mwingine. Hamwezi kumtumikia Mungu pamoja na mali.”

14 Basi Mafarisayo, ambao wenyewe walipenda fedha, waliyasi kia hayo yote wakamcheka. 15 Yesu akawaambia, “Ninyi mnajifa nya kuwa wenye haki mbele za wanadamu, lakini Mungu anaijua mioyo yenu. Kwa maana vile vitu ambavyo wanadamu wanavithamini sana, kwa Mungu havina thamani yo yote.”

Read full chapter