17 Lakini ni rahisi zaidi kwa mbingu na nchi kutoweka kuliko hata herufi moja katika sheria kufutwa.

18 Mtu ye yote anayempa mke wake talaka na kumwoa mke mwin gine anazini, na mwanamume amwoaye mwanamke aliyeachwa na mumewe, ewe, anazini.”

Mfano Wa Tajiri Na Maskini Lazaro

19 Akasema, “Palikuwa na tajiri mmoja aliyevaa nguo za rangi ya zambarau na kitani safi, nguo za gharama kubwa, kila siku.

Read full chapter