Add parallel Print Page Options

12 Aliingia katika mji mdogo, na wanaume kumi walimwendea. Hawakumkaribia, kwa sababu wote walikuwa na ugonjwa mbaya sana wa ngozi. 13 Lakini watu wale wakaita kwa kupaza sauti wakisema, “Yesu! Mkuu! Tafadhali utusaidie!”

14 Yesu alipowaona, akasema, “Nendeni mkajioneshe kwa makuhani.”[a]

Wale watu kumi walipokuwa wanakwenda kujionesha kwa makuhani, waliponywa.

Read full chapter

Footnotes

  1. 17:14 mkajioneshe kwa makuhani Sheria ya Musa ilisema kwamba, kuhani ndiye anayeamua ikiwa mtu mwenye ukoma amepona ukoma wake.