Add parallel Print Page Options

19 Ndipo Yesu akamwambia, “Inuka! Unaweza kwenda. Umeponywa kwa sababu uliamini.”

Kuja Kwa Ufalme Wa Mungu

(Mt 24:23-28,37-41)

20 Baadhi ya Mafarisayo walimuuliza Yesu, “Ufalme wa Mungu utakuja lini?” Yesu akajibu, “Kuja kwa ufalme wa Mungu si kitu unachoweza kuona. 21 Watu hawatasema, ‘Tazama ufalme wa Mungu uko hapa’ au ‘Ule pale!’ Hapana, Ufalme wa Mungu upo hapa pamoja nanyi.”[a]

Read full chapter

Footnotes

  1. 17:21 Mungu upo hapa pamoja nanyi Au “umo ndani yenu”.