14 Nawaambieni, huyu mtoza ushuru alirudi nyumbani akiwa amehesabiwa haki mbele za Mungu na wala si yule Farisayo. Kwa maana ye yote ajikwezaye atashushwa na ye yote ajinyenyekezaye, atainuliwa.”

Yesu Awabariki Watoto Wadogo

15 Watu wakamletea Yesu watoto wao wachanga ili awaguse. Wanafunzi walipowaona, wakawakemea. 16 Lakini Yesu akawaita wale watoto waje kwake, akasema, “Waacheni watoto wadogo waje kwangu, msiwazuie, kwa maana Ufalme wa Mungu ni wa watu walio kama hawa watoto.

Read full chapter