Yesu Aingia Yerusalemu

28 Alipokwisha kusema haya, Yesu alikaa mbele ya msafara akielekea Yerusalemu. 29 Na alipokaribia Bethfage na Bethania kwenye mlima wa Mizeituni aliwatuma wanafunzi wawili akawaagiza hivi, 30 “Nendeni katika kijiji kile kilicho mbele yenu. Mtaka pokuwa mnaingia kijijini, mtamkuta mwana-punda ambaye hajapandwa na mtu bado, amefungwa. Mfungueni, mumlete hapa.

Read full chapter