Add parallel Print Page Options

Yesu Aingia Yerusalemu Kama Mfalme

(Mt 21:1-11; Mk 11:1-11; Yh 12:12-19)

28 Baada ya Yesu kusema mambo haya, aliendelea kusafiri kuelekea Yerusalemu. 29 Akakaribia Bethfage na Bethania, miji iliyo karibu na kilima kinachoitwa Mlima wa Mizeituni. Kisha akawatuma wawili miongoni mwa wafuasi wake, 30 akawaambia, “Nendeni kwenye mji mnaoweza kuuona pale. Mtakapoingia mjini, mtamwona mwanapunda amefungwa ambaye bado mtu yeyote hajampanda. Mfungueni na mleteni hapa kwangu.

Read full chapter