29 Na alipokaribia Bethfage na Bethania kwenye mlima wa Mizeituni aliwatuma wanafunzi wawili akawaagiza hivi, 30 “Nendeni katika kijiji kile kilicho mbele yenu. Mtaka pokuwa mnaingia kijijini, mtamkuta mwana-punda ambaye hajapandwa na mtu bado, amefungwa. Mfungueni, mumlete hapa. 31 Kama mtu akiwauliza, ‘Mbona mnamfungua?’ Mwambieni, ‘Bwana anamhitaji.”’

Read full chapter