33 Petro akajibu, “Bwana, niko tayari kwenda nawe gerezani na hata kufa.” 34 Yesu akamjibu, “Ninakuambia Petro, kabla jogoo hajawika leo usiku, utakana mara tatu kwamba hunijui.”

Kujiandaa Wakati Wa Hatari

35 Kisha Yesu akawauliza, “Nilipowatuma mwende bila mfuko, wala mkoba wala viatu, mlipungukiwa na kitu?” Wakajibu, “La.”

Read full chapter