34 Yesu akamjibu, “Ninakuambia Petro, kabla jogoo hajawika leo usiku, utakana mara tatu kwamba hunijui.”

Kujiandaa Wakati Wa Hatari

35 Kisha Yesu akawauliza, “Nilipowatuma mwende bila mfuko, wala mkoba wala viatu, mlipungukiwa na kitu?” Wakajibu, “La.” 36 Akawaambia, “Lakini sasa, aliye na mfuko au mkoba auchukue. Asiye na upanga, auze koti lake anunue upanga.

Read full chapter