Add parallel Print Page Options

37 Maandiko yanasema, ‘Alidhaniwa kuwa mhalifu.’(A) Maandiko haya lazima yatimizwe. Yaliyoandikwa kuhusu mimi yanatimilika sasa.”

38 Wafuasi wakasema, “Tazama Bwana, hapa kuna panga mbili.”

Yesu akawaambia, “Nyamazeni, acheni mazungumzo ya namna hiyo!”

Yesu Aomba Akiwa Peke Yake

(Mt 26:36-46; Mk 14:32-42)

39-40 Yesu akaondoka mjini akaenda Mlima wa Mizeituni. Wafuasi wake wakaenda pamoja naye. (Alikuwa akienda huko mara kwa mara.) Akawaambia wafuasi wake, “Ombeni ili mtiwe nguvu msije mkajaribiwa.”

Read full chapter