Add parallel Print Page Options

42 “Baba, ukiwa radhi, tafadhali usinifanye ninywe katika kikombe[a] hiki. Lakini fanya unalotaka wewe, siyo ninalotaka mimi.” 43 Kisha malaika kutoka mbinguni akaja akamtia nguvu. 44 Yesu aliomba kwa nguvu zaidi na kustahimili zaidi kama mpiganaji wa mieleka akiwa katika mapambano makali. Jasho kama matone ya damu likadondoka kutoka kwenye uso wake.[b]

Read full chapter

Footnotes

  1. 22:42 kikombe Kikombe ni ishara ya mateso. Yesu alitumia dhana ya kukinywea kikombe akimaanisha kuyakubali mateso ambayo angeyapata katika matukio ya kutisha ambayo yangetokea muda mfupi ujao.
  2. 22:44 Nakala zingine za Kiyunani hazina mstari wa 43 na 44.