43 Malaika kutoka mbinguni akamtokea, akamtia nguvu. 44 Na alipokuwa katika uchungu mkubwa, akaomba kwa bidii zaidi na jasho lake likawa kama matone ya damu ikidondoka ardhini.] 45 Baada ya kuomba, akawarudia wanafunzi wake akawakuta wamelala, wamechoka kwa huzuni.

Read full chapter