52 Kisha Yesu akawaambia makuhani wakuu na wakuu wa walinzi wa Hekalu na wazee waliokuwa wamekuja kumkamata, “Mme kuja na mapanga na marungu, kana kwamba mimi ni jambazi? 53 Kila siku nilikuwa pamoja nanyi lakini hamkunikamata. Lakini wakati huu, ambapo mtawala wa giza anafanya kazi, ndiyo saa yenu.”

Petro Amkana Yesu

54 Wakamkamata Yesu, wakamchukua wakaenda naye nyumbani kwa kuhani mkuu. Petro akawafuata kwa mbali.

Read full chapter