Petro Amkana Yesu

54 Wakamkamata Yesu, wakamchukua wakaenda naye nyumbani kwa kuhani mkuu. Petro akawafuata kwa mbali. 55 Moto ulikuwa umewashwa katikati ya ua, na Petro akaketi na wale waliokuwa wakiota moto. 56 Msichana mmoja mfanyakazi akamwona Petro ameketi karibu na moto. Akamwangalia kwa makini, kisha akasema, “Huyu mtu pia ali kuwa pamoja na Yesu!”

Read full chapter