23 Wote waliokuwepo katika Baraza wakasimama, wakampeleka Yesu kwa Pilato. Wakafungua mashtaka yao kwa kusema: “Tumem wona huyu mtu akipotosha taifa letu. Yeye anawaambia watu wasi lipe kodi kwa Kaisari na kujiita kuwa yeye ni Kristo, mfalme.” Basi Pilato akamwuliza Yesu, “Wewe ndiye mfalme wa Wayahudi?” Yesu akamjibu, “Ni kama ulivyosema.”

Read full chapter