44 Ndipo akamgeukia yule mwanamke akamwambia Simoni, “Unamwona mwanamke huyu? Niliingia nyumbani kwako hukunipa maji ya kunawa miguu, lakini huyu ameniosha miguu kwa machozi yake na kunifuta kwa nywele zake. 45 Hukunisalimu kwa busu, lakini huyu mwanamke amekuwa akiibusu miguu yangu tangu niingie hapa. 46 Hukunipaka mafuta kichwani kama ilivyo desturi lakini huyu mwanamke ameipaka miguu yangu manukato.

Read full chapter