Font Size
Luka 8:12-14
Neno: Bibilia Takatifu
Luka 8:12-14
Neno: Bibilia Takatifu
12 Ile njia zilipoanguka baadhi ya mbegu, ni mfano wa watu wanaolisikia neno la Mungu lakini shetani huja akalichukua kutoka katika mioyo yao, ili wasiamini na kuokolewa. 13 Ile miamba ambamo mbegu nyingine zilianguka ni sawa na watu ambao hufurahia kusikia mahu biri lakini neno la Mungu halipenyi ndani ya mioyo yao. Hawa huamini kwa muda mfupi lakini wanapojaribiwa hupoteza imani yao. 14 Na ile miiba ambamo mbegu nyingine zilianguka ni sawa na wale wanaosikia neno la Mungu lakini baadaye imani yao inasongwa na mahangaiko ya maisha, utajiri, shughuli na anasa; wasiweze kukua.
Read full chapter
Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
Copyright © 1989 by Biblica