14 Na ile miiba ambamo mbegu nyingine zilianguka ni sawa na wale wanaosikia neno la Mungu lakini baadaye imani yao inasongwa na mahangaiko ya maisha, utajiri, shughuli na anasa; wasiweze kukua. 15 Bali ule udongo mzuri ambamo mbegu nyingine zilianguka ni sawa na wale ambao hulisikia neno la Mungu na kulishika kwa moyo mwema na wa utii, wakavumilia na kuzaa matunda.”

Mfano Wa Taa

16 “Ni nani anayewasha taa kisha akaifunika, au akaiweka uvunguni, badala ya kuiweka mahali ambapo mwanga wake utaonekana?

Read full chapter