Add parallel Print Page Options

14 Zilizoanguka katika miiba, zinafanana na watu wanaoyasikia Mafundisho ya Mungu, lakini wanaruhusu wasiwasi, mali na anasa za maisha haya kuwasimamisha na hawaendelei kukua. Hivyo mafundisho hayazalishi matokeo mazuri katika maisha yao.[a] 15 Na zile zilizoangukia katika udongo mzuri, ni wale ambao huyasikia mafundisho ya Mungu kwa moyo safi na mnyoofu. Huyatii na kwa uvumilivu wao huzaa mazao mazuri.

Zingatieni Nuru

(Mk 4:21-25)

16 Hakuna mtu anayewasha taa na kuifunika kwa bakuli au kuificha uvunguni mwa kitanda. Badala yake huiweka kwenye kinara cha taa mahali palipo wazi, ili wanaoingia ndani wapate nuru ya kuwawezesha kuona.

Read full chapter

Footnotes

  1. 8:14 hayazalishi matokeo mazuri … yao Hayazalishi matokeo mazuri katika maisha yao ina maana ya, “kukua kiroho”, ama watu hawa hawafanyi mambo mazuri ambayo Mungu anataka wayafanye.